Nairobi Swahili Poetry

  • Home
  • About
  • Privacy
  • Contact
Home Archive for 2014
Mapenzi haya yetu si ya kwanza
Bali Zamani tulipendana
Ila tulikuwa na wengine wa kutuweka mioyoni yao
Nikiwa naye ni wewe uliyekuwa ndani ya mawazo yangu
Popote niendapo ni wewe ulikuwa kichwani mwangu
Akinibusu sihisi yeye wala ni wewe tuu
Siwezi mueleza kwa woga wa kuvunjy mwoyo wake
Sina Uwezo wa kukaa mbali na wewe
  Tangu nianze kukupenda
Sijawahi kuhisi vile nahisi wakati huu
Mawazo kuhusu penzi hili letu hunipotezea usingizi
Siwezi pata raha ikiwa uko mabali na mimi
Sina uwezo wa kupenda mtu mwingine yeyote
Kiasi tunavyopendana
Hakuna yule aweza kupima
Nyimbo zote hazina maana yeyote
Ikiwa uko mabali na mimi
Kila siku ni siku ya mapenzi yetu
Sina Uwezo wa kubusu mwingine ila wewe
Kwa maana sijawahi kupendwa vile unavyo nipenda
Nakuahidi kuwa sikuwachi milele
Hata dunia iwe mwisho wa maisha
Sitakuwa bila wewe
Sina Uwezo wa kuishi peke yangu
Wewe ni maji ambayo humaliza kiu
Huosha uchovu wowote
Na kunipa raha tele
Mimi na Wewe hatuwachani kamwe
Sina Uwezo wa kupumua bila mahaba yako
Siwezi kutulia ila kwa busu lako tamu

Maisha hayawezi kunitoa kwa moyo wako
Jana usiku ilikuwa mwisho wa huzuni
Uliniweka katika hali ya kucheka na kutulia kwa roho yako
Mapenzi unayonipa yanifanya nipepee
Kama yule kipepeo mweupe tuliyemuona nje ya nyumba
Sitarudi nyuma wala kuwa na wasiwasi wowote
Kule tunapoenda ni muhimu kuliko tuliko toka
Mabali tujafika lakini mimi na wewe
Hakuna lolote laweza kutushinda
Nimekubali kuwa wako milele
Mvua ikinyesha wale ukame uwe ni mimi na wewe tuu
Busu la asubuhi huniamsha kutoka usingizini
Nikifungua macho nikuone kando yangu
Najua niko na pendo lako
Hakuna mtu aweza kutupatanisha duniani
Asali ni tamu lakini sio kuliko mahabu uliyo nipa
Ukiuliza nitakueleza
Nakupenda pia
Nalia machozi ya furaha kwani najua wanipenda sana
Wewe ndiwe nimechagua kuishi naye hadi mwisho wa dunia
Nyimbo za mapenzi zimeimbwa ma wana muziki
Hakuna yule anaweza kueleza mapenzi haya yetu
Nakupenda bila woga wowote
Najua wanipenda pia
 
Natafuta penzi lako
Busu lako lanitia wazimu
Natamani uwe wangu
Usiniache na kiu baada ya kuniloweza
Maisha naishi kwa upendo wako
Lepe la usingizi sipati usiku wote
Mchana nakuhitaji
Kama ardhi inavyotamani maji jangwani
Roho yaniuma ukienda
Nyumba yako ni ndani ya roho yangu
Nakupenda hadi siwezi kueleza
Ulinionjesha
Mahaba yako
Ukanifanya niwe wako milele
Nakupa kiasi cha roho yangu
Unieleze kwa nini nakupenda
Utamu wa pendo lako
Hunimaliza mzima mzima
Nguvu hunitoweka
Unapo nikumbatia
Heshima yako ndio nataka
Kujaza mapenzi yetu
 
Nakutuliza moyoni
Ulinipenda na roho yako yote
Ukanipa mahaba ya kutosha
Ambayo yaniloweza hadi sitamani yaishe
Penzi lako latuliza mawazo yangu
Mvua ikinyesha
Giza likiingia mawinguni
Unawasha taa na pendo lako
Na kufukuza upweke
Busu lako no tamu
Tamu zaidi ya tunda lolote duniani
Nakutaka
Nakuhitaji
Nipe ruhusa yako
Nikuweke moyoni milele
Dhahabu haiwezi kulinganisha
Jinsi tunavyopendana
Hata ukame uwepo, theluji inyeshe
Mimi na wewe ni hisia moja
Nahisi utupu ndani ya nafsi yangu
Sababu yangu bila wewe
Haina maana kwangu
Nazama na uzito wa pendo lako
Kila unaponituliza
Unanivuta kwa upweke wako
Hakuna kinachonitosheleza
Ila joto la mahaba yako
Mpenzi wa roho yangu
Mapenzi haya yako
Siyajui
Nikikutazama machoni
Machozi hunidondokea
Nikumbatie
Hadi upweke wote uishe
Kama maji baridi
Yanavyotiririka mwilini
Wewe hunituliza vilivyo
Waridi la moyo wangu
Milele hunyauki
Muujiza wa maisha yangu
Utamu wa pendo lako
Hunitembeza jangwani
Mikono yako iliundwa
Kunifunika mimi peke yangu
Ndotoni sikosi kukutazama
Nifunguapo macho
Mbele yangu hutoki


Mapenzi unayonipa
Sijawahi kupata
Tazama machoni mwangu
Huwezi kupotea maishani
Milele
Mimi na wewe ni hisia moja
Popote niendapo mafikira yangu ni kwako tu
Sijawahi kupende jinsi ninavyo kupenda
Sijawahi kupendwa jinsi unavyo nipenda
Busu lako hunifanya wazimu
Hadi sitamani uniwache kamwe
Subscribe to: Comments ( Atom )

LATEST POSTS

  • Nakupenda Pia
    Maisha hayawezi kunitoa kwa moyo wako Jana usiku ilikuwa mwisho wa huzuni Uliniweka katika hali ya kucheka na kutulia kwa roho ...
  • Sina Uwezo
    Sina Uwezo wa kukaa mbali na wewe   Tangu nianze kukupenda Sijawahi kuhisi vile nahisi wakati huu Mawazo kuhusu penzi hili letu huni...
  • Milele
    Mapenzi unayonipa Sijawahi kupata Tazama machoni mwangu Huwezi kupotea maishani Milele Mimi na wewe ni hisia moja Popote ...
  • Mapenzi yako
    Mpenzi wa roho yangu Mapenzi haya yako Siyajui Nikikutazama machoni Machozi hunidondokea Nikumbatie Hadi upweke wote ui...
  • Mapenzi yetu
      Natafuta penzi lako Busu lako lanitia wazimu Natamani uwe wangu Usiniache na kiu baada ya kuniloweza Maisha naishi kwa up...
  • Ni wewe
      Nakutuliza moyoni Ulinipenda na roho yako yote Ukanipa mahaba ya kutosha Ambayo yaniloweza hadi sitamani yaishe Penzi lak...
  • Penzi langu
    Nahisi utupu ndani ya nafsi yangu Sababu yangu bila wewe Haina maana kwangu Nazama na uzito wa pendo lako Kila unaponituliz...
  • Zamani Tulipendana
    Mapenzi haya yetu si ya kwanza Bali Zamani tulipendana Ila tulikuwa na wengine wa kutuweka mioyoni yao Nikiwa naye ni wewe uliyekuw...

Categories

  • Mapenzi yako
  • Mapenzi yetu
  • Milele
  • Nakupenda Pia
  • Ni wewe
  • Penzi langu
  • Sina Uwezo
  • Zamani Tulipendana

Blog Archive

  • ▼  2014 (8)
    • ▼  October (1)
      • Zamani Tulipendana
    • ►  September (7)
      • Sina Uwezo
      • Nakupenda Pia
      • Mapenzi yetu
      • Ni wewe
      • Penzi langu
      • Mapenzi yako
      • Milele
Powered by Blogger.
Copyright 2014 Nairobi Swahili Poetry.
Designed by OddThemes