Sina Uwezo

Sina Uwezo wa kukaa mbali na wewe
  Tangu nianze kukupenda
Sijawahi kuhisi vile nahisi wakati huu
Mawazo kuhusu penzi hili letu hunipotezea usingizi
Siwezi pata raha ikiwa uko mabali na mimi
Sina uwezo wa kupenda mtu mwingine yeyote
Kiasi tunavyopendana
Hakuna yule aweza kupima
Nyimbo zote hazina maana yeyote
Ikiwa uko mabali na mimi
Kila siku ni siku ya mapenzi yetu
Sina Uwezo wa kubusu mwingine ila wewe
Kwa maana sijawahi kupendwa vile unavyo nipenda
Nakuahidi kuwa sikuwachi milele
Hata dunia iwe mwisho wa maisha
Sitakuwa bila wewe
Sina Uwezo wa kuishi peke yangu
Wewe ni maji ambayo humaliza kiu
Huosha uchovu wowote
Na kunipa raha tele
Mimi na Wewe hatuwachani kamwe
Sina Uwezo wa kupumua bila mahaba yako
Siwezi kutulia ila kwa busu lako tamu

Share this:

ABOUT THE AUTHOR

Hello We are OddThemes, Our name came from the fact that we are UNIQUE. We specialize in designing premium looking fully customizable highly responsive blogger templates. We at OddThemes do carry a philosophy that: Nothing Is Impossible

0 comments:

Post a Comment